Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu anasema Yusuf Keynan (aliyefanya kazi katika redio Mustaqbal), alikuwa mwandishi wa habari kijana aliyekuwa akipendwa na hodari katika kazi yake.
Huyo ni mwandishi wa habari wa kwanza kuuwawa nchini Somalia mwaka huu, baada ya waandishi habari kadha kuuwawa kwa mfululizo katika miaka miwili iliyopita.
Shirika la Kuwalinda Waandishi wa Habari linasema kuwa Somalia ni moja kati ya nchi hatari kabisa kwa waandishi.
Hata hivyo hakuna aliyedai kuhusika na mauaji ya kijana huyo, hadi hivi sasa..
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.