Mshambuliaji matata wa timu ya soka ya Uruguay Luis
Suarez anakabiliwa na marufuku ya mda mrefu itakayomlazimu kukosa mechi
nyengine za michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya
kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.
Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha
harakati za kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila
dhidi ya Italy siku ya Jumanne.Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.
Suarez na Chiellini
Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho,lakini FIFA bado inaweza kumuadhibu Suarez.
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa mechi zote za kombe hilo zilizosalia.
Raia huyo wa Denmark ameliambia gazeti la Liverpool la Echo kwamba '' nina hakika FIFA itachukua swala hilo la Suarez kama mfano kwa wengine''.
''Ni dhahiri kwamba matumaini yake ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia iliosalia yamekwisha na ninataraji kwamba FIFA itampatia marufuku ya mda mrefu''.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.