Sababu kubwa zilizotolewa na Vatican, ni kwamba hali ya kiongozi huyo wa wakatoliki kote duniani anahitaji muda mkubwa zaidi wa kupumzika, hivyo imemlazimu afuate ushauri wa Mganga wake!.....
Huko Ujerumani, msemaji wa serikali
amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu aliyezaliwa katika
Jimbo la Bavaria la nchini humo.
Baba Mtakatifu ameelezea kwamba
matatizo ya kiafya yamemfanya kutangaza kujiuzulu
Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron, amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano baina ya
Vatican na Uingereza.
Askofu mkuu wa Canterbury amesema
amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa
undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela
Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa,
waislamu na wayahudi.
Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru
bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.
Uwamuzi na hatua ya Papa Benedict
XVI wa kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka minane
akiongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi
kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.
Makao makuu ya Kanisa Katoliki huko
Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa
tatu, na sherehe za Pasaka.
Tabia ya kujiuzulu kwa Papa si
ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi karibuni.
Mwandishi wa BBC mjini Roma Alan
Johnston anasema habari hizi zimetokea kama radi, na kwamba hakukua natetesi
yoyote juu ya uwezekano kama huu.
Msemaji wa Vatikani Father Federico
Lombardi, amesema kuwa hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa na fununu
juu ya tukio hili.
Kakake Papa huyu mzaliwa wa Ujerumani
alipewa ushauri na Daktari wake asifanye ziara nyingine yoyote ya Marekani na
kwamba kwa miezi kadhaa Mtakatifu Papa amekuwa akitafakari kujiuzulu.
Akizungumza kutoka nyumbani kwake
huko Regensburg, Ujerumani, Georg Ratzinger amesema kuwa Kaka yake alikuwa
ameanza kupata shida ya kutembea na kwamba kujiuzulu kwake ni hatua ya
kimaumbile.
Wakati wa kutawazwa kama Papa,
Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa akiwa
mwenye umri mkubwa wa miaka 78.
Alitangazwa Papa mnamo mwezi Aprili
2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa
wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha miongo
mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana.
Katika taarifa yake, Mtakatifu Papa
amesema: "baada ya kujichunguza binafsi na nafsi yangu mbele ya Mola
wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya, ukiambatana na umri mkubwa,
ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Kuna kipengele katika sheria ya
Kanisa kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho
kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki.
|
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.