Askofu aliyedumu kwenye
nafasi ya Uaskofu zaidi ya Miongo Mitatu, Askofu Thomas Laizer amefariki jioni
ya leo Katika Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa wa Arusha. Askofu Thomas Laizer
amefikwa na mauti hiyo baada ya kuugua na....
kukaa Hospitalini hapo zaidi ya mwezi
Mmoja.
Askofu Laizer amefariki huku Dayosisi Ya Kaskazini ya Kanisa la
KKKT ikiwa inamuhitaji pamoja na busara zake kuweza kutatua mgogoro
unaolikabili Kanisa hilo kwa sasa kufuatia deni la mabilioni kadhaa.
Askofu Laizer alianza kuugua mapema mara baada ya mgogoro kuanza
kushika hatamu, haijafahamika moja kwa moja kama ugonjwa wa Baba Askofu una
uhusiano wa moja kwa moja na mauti iliyomfika.
Baba Askofu Laizer atakumbukwa kwa ujasiri wake wa
kuikosoa Serikali pasipo woga, lakini puia atakumbukwa sana Kipindi cha Babu Wa
Loliondo na Kikombe chake Cha Tiba.
|
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.