 |
Hayati Pope Shenouda.. | |
Baraza la maaskofu wa Kikopti nchini
Misri, linatarajiwa kumpigia kura mrithi wa papa Shenouda wa tatu aliyefariki
mwezi Machi.
Maaskofu wawili na watawa watatu
wako kwenye orodha ya.....
wale wanaogombea wadhifa huo ambapo yeyote atakayeshinda
atakuwa kiongozi wa miamoja na kumi na nane kuongoza madheheyo hayo ambayo ndio
kundi ndogo sana la wakristo duniani.
Baraza hilo litachagua wagombea
watatu na kuandika majina yao kwenye vijikaratasi ambavyo vitawekwa kwenye boxi
katika mimbar ya kanisa la mtakakatifu Mark, mjini Cairo.
Kisha mtoto atakayekuwa amefumbwa
macho, atachukua kijikaratasi kimoja kutoka kwenye boxi hilo, jina la atakekuwa
amechukua ndiye atakuwa Papa mpya.
Atayakuchaguliwa ataapishwa katika
sherehe itakayofanyika tarehe 19 mwezi Novemba.
Papa Shenouda wa tatu aliongoza
waumini wa kanisa hilo nchini Misri kwa miongo minne na alifariki akiwa na umri
wa miaka 88 mwezi Machi, baada ya kuugua saratani.
Aliwataka maafisa wa kanisa hilo
kufanya kila wawezalo kushughulikia maswala muhimu ya waumini wa kanisa hilo
baada ya mashambulizi kadhaa dhidi ya makanisa katika miaka ya hivi karibuni.
Mrithi wake anakabiliwa na kibarua
cha kuwahakikishia kuimarika kwa imani jamii ya waumini wa kanisa hilo hasa
wakati huu ambapo harakati za makundi ya kiisilamu zimeshika kasi nchini Misri.
Vijana wengi wa kikopti watakuwa
wanatazamia kupata kiongozi atakayewasaidia kuweka bayana majukumu yao chini ya
utawala usio kuwa wa Mubarak.
 |
Pope Shenouda.. |
 |
Msafara wa maziko ya Pope Shenouda.. |
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.