![]() | |||||||
Rais Omary Al-Bashir wa Sudan ya Kaskazini...... |
Shambulizi dhidi ya kiwanda cha
Sudan liliwaua watu wawili,Sudan imesema kuwa inapanga kuishtaki Israel kwa
Umoja wa Mataifa kuhusiana na madai ya shambulizi dhidi ya kiwanda chake cha
silaha mjini Khartoum.
Balozi wa Sudan katika Umoja wa
Mataifa Daffa-Alla Elhag Ali Osman, amesema kuwa.....
Israel imevamia kiharamu anga
zake mara tatu katika miaka ya hivi karibuni.
Sudan hata hivyo bado haijatoa
ushahidi wowote kuunga mkono madai yake na Israel nayo haijatoa tamko lolote
kuhusu madai hayo dhidi yake.
Duru nchini Sudan zinasema kuwa
kiwanda hicho kilimiaminika kuendeshwa na Iran.
Mwandishi wa BBC w amaswala ya
ulinzi anasema inaaminika kuwa kiwanda hicho kilikuwa kinatengeza roketi na
zana zengine kwa niaba ya Iran ili kuzipeleka kwa wapiganaji wa Hamas.
Na kwa hivyo Israel iliona umuhimu
wa kusitisha shughuli za kiwanda hicho nchini Sudan badala ya kuchukua hatua
ambazo zingeudhi Misri.
Ingawa srael bado haijatoa tamko
lolote kuhusu madai ya Sudan, afisaa mmoja wa ulinzi aliambia vyombo vya habari
kuwa Sudan ni nchi hatari ya kigaidi.
''Serikali ya Sudan inaungwa mkono
na Iran na inatumiwa kama kivukio cha silaha kupitia Misri na kuingia Hamas
pamoja na kuyaendea makundi mengine ya kigaidi. '' alisema afisaa huyo.
Mwezi Aprili mwaka jana,Khartoum
ilidai kuwa Israel ilihusika na shambulizi lengine la angani dhidi yake ambalo
liliwaua watu wawili karibu na mji wa Port Sudan.
Israel pia ililaumiwa kwa shambulizi
lengine dhidi ya msafara wa magari Kaskazini Mashariki mwa Sudan mwaka 2009.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.