Aliyekuwa bawabu wa Papa Benedict
amerejea mahakamani katika kile kinachotarajiwa kuwa siku muhimu kabisa ya kesi
yake mjini Vatican kwa mashtaka ya wizi wa....
nyaraka muhimu za siri kutoka ofisi
ya Papa.
Nyaraka hizo zimefichua tuhuma za
rushwa na mgogoro wa madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki.
Bawabu huyo Paolo Gabriele,
anatarajiwa kutoa ushahidi hii leo ikiwa ni siku ya pili ya kesi hiyo.
Makao makuu ya kanisa hilo Vatican
wanasema kuwa Gabriele tayari amekiri mashtaka akisema kuwa alitaka tu kuweka
hadharani uovu na rushwa ndani ya kanisa hilo.
Bwana Gabriele anakabiliwa na adhabu
ya kifungo cha miaka minne jela iwapo atapatikana na hatia.
![]() |
Paolo Gabriele akiwa ameketi mbele, wakati Pope akipungia waumini kutokea ndani ya gari.. |
![]() |
Paolo Gabriele, aliyezungushiwa kiduara akimuwekea maji ya kunywa Pope Benedict wa 16, wakati huo akiwa bado kazini. |
![]() |
Paolo Gabriele |
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.