Sheria kali itakayowashurutisha
waumini wa kikatoliki kulipa kodi ya kanisa la sivyo wanyimwe sakramento
imepitishwa nchini Ujerumani.
Maaskofu waliopitisha sheria hiyo
wamesema kuwa yeyote atakayekosa kulipia kodi ya kanisa ambayo ni asilimia........
nane
ya mapato yao watanyimwa sakramento na kisha kutotambuliwa kama wakatoliki.
Maaskofu hao wameshtushwa na idadi
ya watu wanaoendelea kuasi ukatoliki.
Wanasema kuwa hatua kama hii ya
kuasi dini itakuwa ni kwenda kinyume kabisa na maadili ya jamii.
Watu wote waliosajiliwa rasmi kama
wakatoliki, waprotestandi au wayahudi, hulipa asilimia 8 hadi 9 ya mapato yao
ya kila mwaka.
Kodi hiyo ilianza kutozwa karne ya
19 kama fidia ya kutaifishwa kwa mali ya kanisa nchini humo.
Idadi ya wakatoliki nchini Ujerumani
ni asilimia 30, lakini idadi ya watu nchini Ujerumani wanaoasi kanisa hilo
iliongezeka hadi watu 181,000 mnamo mwaka 2010, huku lawama zikitolewa kwa
kashfa nyingi za ngono zilizokumba kanisa hilo wakati huo.
Maaskofu hao wamechukua hatua baada
ya kushtushwa na ongezeko la waumini wa kanisa hilo wanaoasi dini, pamoja na
profesa mmoja aliyestaafu Hartmut Zapp kutangaza mwaka 2007 kuwa kamwe hatalipa
kodi hiyo ingawa atasalia kuwa muumini wa kikatoliki.
Iliarifiwa kuwa profesa huyo alitaka
kuendelea kupokea sakramento na kuandelea kutambulika kama mkatoliki ingawa
maaskofui walipinga hilo na sasa kesi kati ya profesa huyo na kanisa
itafikishwa mahakamani siku ya Jumatano.
 |
Kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Duniani, Papa Benedict wa kumi na sita akimdhibitisha Cardinal wa Germany.. |
 |
Papa Benedict wa kumi na sita.. |
 |
Papa Benedict.. |
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.