 |
Askofu mkuu anayestaafu Rowan Williams | |
Jopo la
wanachama wakuu wa kanisa la Kianglikana wanakutana leo kumchagua askofu mkuu
mpya wa Canterbury kuongoza kanisa hilo.
Wadadisi wanasema kuwa
kawaida huwa kuna idadi kubwa ya wagombea wanaoweza..
kuchukua nafasi ya Askofu
mkuu anayestaafu Rowan Williams hali inayoifanya vigumu kujua nani
atakayechukua wadhifa wenyewe.
Askofu mpya atachukua uongozi
wakati kanisa hilo linakumbwa na migawanyiko kuhusu maswala kadhaa mfano, ikiwa
askofu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja anaweza kutawazwa kama askofu pamoja
na kudidimia kwa idadi ya wafuasi wa kanisa hilo kila kukicha.
Jopo hilo litakutana kwa siku
tatu kabla ya kuwasilisha jina la askofu mpya.
 |
Askofu Rowan Williams |
 |
Askofu Rowan Williams |
 |
Kanisa la Canterbury.. |
 |
Kanisa la Canterbury.. |
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.