Ripoti kutoka Magharibi mwa Afrika zinasema kuwa sherehe za Eid Ul Adhaa zimeathiriwa vibaya na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Nchini Guinea maeneo ya uma ambapo watu hukongamana ili kufanya ibada yalikuwa bila watu.
Nchini Sierra Leone Muungano wa baraza la maimamu uliwaonya waislamu kutoamkuana kwa kushikana mikono wala kukumbatiana.
Madaktari
nchini Ujerumani wanasema kuwa mwanasayansi aliyeambukizwa ugonjwa wa
ebola wakati alipokuwa akilifanyia kazi shirika la afya duniani
ameponea.
Vilevile Muunguzi wa Ufaransa aliyeambukizwa ugonjwa huo
alipokuwa akijitolea katika shirika la madaktari wasio kuwa na mipaka
MSF nchini Liberia pia ameponea.
Takriban watu 3400 wamefariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo. |
0 comments:
Post a Comment