![]() |
Papa mpya ni Askofu Tawadros |
Kanisa la Copt la Misri limemchagua
papa mpya atayewaongoza Wakristo wanaokisiwa kuwa milioni-8 nchini Misri.
Papa mpya ni Askofu Tawadros mwenye
umri wa miaka 60, na alikuwa......
msaidizi wa Papa Shenouda wa tatu ambaye alifariki
mwezi wa March baada ya kuongoza kanisa hilo kwa miaka 40.
Jina la Askofu Tawadros liliteuliwa
na mtoto kati ya majina matatu yaliyoandikwa kwenye vikaratasi vilivowekwa
kwenye jagi.
Uteuzi huo ulitokea katika ibada maalumu
iliyofanywa katika Kanisa la Saint Mark's mjini Cairo.
Mwandishi wa BBC mjini Misri anasema
papa mpya ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na maarifa ya uongozi; na kwamba
atahitaji sifa hizo katika nchi ambayo inajadili mchango wa Uislamu baada ya
mapinduzi yaliyomtoa madarakani Rais Hosni Mubarak.
Msemaji wa chama cha Muslim
Brotherhood, kinachoongoza serikali, alinena kuwa wana matumaini kwamba
watakuwa na ushirikiano na papa mpya.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.