"Iron Dome" ni
mmojawapo ya kinga nyingi inayomilikiwa na Israel, na inayotumika dhidi ya
makombora.
Mfumo huo unatumia rada ili kufuata
makombora yanayorushiwa Israel, halafu...
hufyatua makombora yake ili kuangamiza
hayo yanaoyojaribu kupenya.
Mfumo huu ulichukua miaka mingi
kujenga na ulianza kutumika mapema 2011.
"Iron Dome" imesifiwa sana
na jeshi la Israel katika mashambulizi yanayoendelea huko Gaza.
Ilipofika Jumamosi iliyopita jioni,
kinga hiyo ilikuwa imeshazuia makombora 245 toka Gaza katika muda wa siku tatu,
kulingana na habari za kijeshi.
Hata hivyo inaonekana kwamba
wapinzani wa Gaza wanazidi kuboresha silaha zao.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.