Dr.KAWAMBWA KUKUTANA NA WADAU WA ELIMU KESHO..
Waziri wa elimu na ufundi Dr.Shukuru Kawambwa, kesho atakutana na Maafisa elimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara, ili kukumbushana na kupeana mikakati ya....
kuboresha elimu zaidi katika sehemu zao za kazi.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar-es-salaam.
Lakini pia, keshokutwa yaani Alhamisi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo jirani na Viwanja vya Gymkhana, Waziri Kawambwa Atakuwa anakutana na wadau mbalimbali wa elimu ili kuweza kupata mawazo na njia mpya za kuweza kuboresha elimu ya Tanzania, na mkutano huo utaanza saa mbili na nusu asubuhi.. hii ni kwa mujibu wa msemaji wa Wizara hiyo alipozungumza nami jioni ya leo (Bw.Bunyanzi Ntambi)
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.